• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka yasema hifadhi za viumbe za Tanzania ni ufunguo wa kulinda mazingira

    (GMT+08:00) 2019-08-29 08:46:27

    Mamlaka ya Tanzania imesema hifadhi tano za nchi hiyo ndio ufunguo wa kulinda mazingira, pia zinabeba jukumu kubwa katika maendeleo ya uchumi na kijamii.

    Akifungua mkutano wa sayansi kuhusu mtu na hifadhi za viumbe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Utumishi na Utawala Bora TAMISEMI, George Simbachawene amesema katika kutambua umuhimu wa hifadhi za viumbe, Tanzania imekuwa ikitekeleza mpango wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO unaohusu mtu na hifadhi za viumbe. Amebainisha kuwa Tanzania ina hifadhi tano ambazo zina utajiri anuwai wa maliasili na mfumo wa ikolojia unaofanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi kubwa zaidi 12 zenye uanuwai mkubwa wa viumbe duniani.

    Hata hivyo amesema hifadhi hizo zinakabiliwa na changamoto za kiusimamizi zisizo za kawaida, zikiwemo ukuaji wa kasi wa idadi ya watu ndani na maeneo ya nje ya hifadhi, ambao unapelekea kuongezeka kwa mahitaji ya rasilimali na kutoa shinikizo kwenye msingi wa maliasili zilizopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako