• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Zimbabwe yaelemewa na wingi wa wafungwa magerazani

  (GMT+08:00) 2019-08-29 08:46:45

  Shirika la habari la Zimbabwe New Ziana limeripoti kuwa Magereza ya Zimbabwe yameelemewa na wafungwa na hivi sasa yanabeba wafungwa elfu 19, 500, idadi ambayo imezidi uwezo wa kawaida wa wafungwa 17,000.

  Likimnukuu waziri wa Mambo ya Sheria, Haki na Bunge Ziyambi Ziyambi, shirika hilo limesema, hata hivyo serikali haijafikiria kutoa msamaha wowote kwa wafungwa ili kupunguza mzigo wa magereza. Mapema mwaka jana rais Emmerson Mnangagwa aliwasamehe wafungwa 3,000 chini ya msamaha wa rais katika juhudi za kupunguza idadi ya wafungwa. Hivyo waziri Ziyambi amesema toka hapo serikali imegundua kuwa msamaha wanaopewa wafungwa hausaidii kupunguza idadi yao magerezani. Badala yake amesema serikali itatoa kipaumbele katika kuwekeza kwenye magereza mapya nchi nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako