• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNESCO yasema Afrika inapaswa kuingiza masomo ya utumwa kwenye mtaala wa elimu

    (GMT+08:00) 2019-08-29 08:47:05

    Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limezitaka nchi za Afrika kufikiria kuingiza masomo ya biashara ya utumwa ya kupitia bahari ya Atlantiki katika mtaala wao wa elimu.

    Mwakilishi wa UNESCO nchini Ghana Abdourahamane Diallo, amesema ni muhimu kuelimisha vizazi vipya juu ya historia nzima ya utumwa, athari zake barani Afrika na vizazi vya utumwa wa Afrika, ili kuleta mchakato wenye ufanisi wa kupona. Amesema ni uamuzi huu uliotolewa na Umoja wa Afrika kwamba nchi zote wanachama zitumie mradi wa utumwa kwenye elimu, lakini nchi zimekuwa nzito sana kutekeleza.

    Ameitaka Ghana ambayo inaufanya mwaka 2019 kama Mwaka wa Kurejea kwa Vizazi vya Utumwa Afrika, kutumia sherehe hizi kuongoza ajenda hii, ili vizazi vipya vijue kilichotokea na kulinda kisijirejee tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako