• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwezekezaji wa China azindua kiwanda kikubwa zaidi cha nepi cha Afrika Mashariki nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2019-08-29 08:52:51

  Wawekezaji wa China wamezindua kiwanda kikubwa zaidi cha nepi cha Afrika Mashariki nchini Kenya.

  Mkurugenzi wa kiwanda cha Kampuni ya Viwanda ya Sunda ya Kenya Huang Shiwei amesema, kiwanda hicho cha utengenezaji kilichowekezwa shilingi bilioni 4 za Kenya, kina eneo la ekari 35 huko Mavoko, kilomita 30 Kusini Magharibi mwa Nairobi.

  Huang amesema, mahitaji ya nepi nchini Kenya kila mwaka ni karibu milioni 800.

  Kwa mujibu wa kiwanda hicho cha nepi, faida moja ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kwamba, Kenya itaokoa fedha za kigeni zinazotumika kununua nepi kutoka nchi za nje.

  Wakati huo huo, kiwanda hicho kitatoa nafasi 300 za ajira kwa wenyeji wa huko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako