• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zahimizwa kukumbatia sera shirikishi za dijitali ili kuwanufaisha wasichana wasiokwenda shule

    (GMT+08:00) 2019-08-29 09:06:04

    Wataalamu wa Afrika wanaojihusisha na mageuzi ya kidijitali, jinsia na elimu wamezihimiza nchi za Afrika na taasisi za Umoja wa Afrika kukumbatia sera shirikishi za dijitali ili kuwanufaisha mamilioni ya wasichana wasiokwenda shule kote barani humo.

    Taarifa iliyotolewa jana na Umoja wa Afrika inasema, wito huo umetolewa kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kibara ulioandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Umoja wa Afrika kuhusu Elimu ya Wasichana na Wanawake wa Afrika.

    Mkutano huo wenye kaulimbinu "Kupanua fursa za wasichana wasiokwenda shule kupitia mageuzi ya kidijitali", umesisitiza kuwa teknolojia za kisasa za Tehama ni nyenzo zenye nguvu katika kutatua suala la mamilioni ya wasichana na wanawake wasiokwenda shule barani Afrika.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Umoja wa Afrika, juhudi za pamoja kwenye sekta ya Tehama zitaweza kuwasaidia wasichana na wanawake milioni 53 wa Afrika wasiokwenda shule kukabiliana na changamoto za maisha na kutimiza ndoto zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako