• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera ya China ya kufungua mlango yatajwa kuleta manufaa

    (GMT+08:00) 2019-08-29 09:06:24

    Jopo la washauri bingwa nchini Zambia limesema sera ya China ya kuendeleza mageuzi na kufungua mlango imechangia kujitokeza kwa uchumi wake na kuongezeka kwa ushawishi wake kwenye biashara ya kimataifa.

    Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha utafiti wa sera nchini Zambia Bi. Bernadette Deka-Zulu amesema mafanikio ya sasa yanayoonekana nchini China yanatokana na sera yake ya ufunguaji mlango kwa nje katika ngazi ya pande mbili na pande nyingi.

    Amesema, imekuwa ngumu kwa nchi yoyote kuipuuza China kwa kuwa China imekuwa ikiongoza katika biashara ya kimataifa wakati nchi nyingi duniani zinategemea maendeleo ya viwanda nchini China.

    Bi. Deka-Zulu pia amesema sasa ni wajibu wa vijana wa China na Zambia kuendeleza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili ili kuhakikisha unaendelea kupiga hatua mbele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako