• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikosi cha ulinzi cha Jeshi la China mkoani Hong Kong chamaliza kazi ya kubadilisha askari wake kwa mara ya 22

  (GMT+08:00) 2019-08-29 19:36:36

  Kikosi cha ulinzi cha Jeshi la China mkoani Hong Kong leo limekamilisha kazi ya kubadilisha askari wake kwa mara ya 22 tangu kikosi hicho kilipowekwa mkoani Hong Kong mwaka 1997.

  Hatua hiyo iliyoidhinishwa na Kamati kuu ya kijeshi, ni ya kawaida na inaendana na sheria ya China kuhusu kikosi hicho kwenye mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong.

  Askari wapya wamefika kwenye kikosi hicho kwa njia ya ardhi, bahari na anga. Askari hao wamepewa mafunzo na masomo ili kuwa na uwezo wa kijeshi na ufahamu kuhusu hali ya jumla ya Hong Kong na sheria husika.

  Kikosi hicho kimetoa ahadi ya kufuata kikamilifu amri za Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na kamati ya kijeshi, na kutekeleza kikamilifu utaratibu wa "nchi moja, mifumo mwili", sheria ya msingi ya Hong Kong na sheria kuhusu kikosi cha ulinzi cha jeshi la China mkoani Hong Kong.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako