• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki Kuu ya Ulaya yasema benki 24 zitahamishiwa kwenye maeneo ya Euro kutoka London

    (GMT+08:00) 2019-08-29 19:41:01

    Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa Benki Kuu ya Ulaya Bw. Andrea Enria amesema ili kukabiliana na Brexit, benki 24 zitahamia kwenye maeneo ya Euro kutoka London, na inatarajiwa kuwa idadi ya uhamasisha wa fedha itafikia Euro trilioni 1.3, kati ya benki hizo, saba zitasimamiwa na Benki Kuu ya Ulaya moja kwa moja.

    Bw. Enria ameongeza kuwa Benki Kuu ya Ulaya na ya Uingereza zimehimiza benki za Uingereza kufanya maandalizi yote mapema ikiwemo kuomba leseni, kuhamisha mali kwa utaratibu, kuthibitisha mfumo wa uendeshaji, na kuanzisha matawi mapya katika Umoja wa Ulaya.

    Bw. Enria anaona ingawa benki husika zinaweka mpango wa dharura, Brexit itasababisha mtikisiko kwa soko la fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako