• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China ina uwezo wa kukabiliana na mgogoro wa kibiashara

  (GMT+08:00) 2019-08-29 19:42:42

  Baada ya raundi ya tatu ya hatua za kulipiza kisasi iliyochukuliwa na China, baadhi ya wamarekani wametangaza kuongeza zaidi ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 550 zinazouzwa nchini Marekani, na kujaribu kuilazimisha China isalimu amri kwa njia ya kuishinikiza. Lakini kwa mara nyingine tena, imepima kwa makosa nia na uwezo wa China. Kwani nia ya China katika kulinda maslahi makuu ya nchi na maslahi ya kimsingi ya wananchi haitaweza kuvunjika, na ina uwezo wa kukabiliana na athari mbaya zinazotokana na mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani.

  Katika mwaka uliopita, China ililazimika kulipiza kisasi kwa raundi ya tatu kutokana na mikwaruzano ya biashara iliyochochewa na Marekani na kuzidi kupamba moto. Hii ni hatua ya lazima inayochukuliwa na China kwa ajili ya kulinda maslahi yake halali, pia ni kitendo cha lazima katika kulinda utaratibu wa biashara wa pande nyingine na kanuni za kimataifa. Kama China ilivyosisitiza mara kwa mara kwamba, hakuna mshindi katika vita vya biashara, China haipendi kufanya vita vya biashara, lakini pia haiogopi kufanya hivyo, na itafanya wakati unapohitajika. Kila mara Marekani inapotoa shinikizo kwa kushika fimbo ya ushuru na kujaribu kuilazimisha China isalimu amri, inashindwa kila mara. Ingawa China ililazimika kuchukua hatua za kulipiza kisasi, lakini inachukua hatua za kujibu kwa msimamo wa kimantiki.

  Jumuiya ya kimataifa inaunga mkono msimamo wa China. Kama mkurugenzi wa zamani wa Idara ya sera za uchumi na biashara ya London, Uingereza John Ross alivyodhihirisha kuwa, hatua za kulipiza kisasi zilizochukuliwa na China ni jibu la lazima dhidi ya Marekani kuongeza zaidi ushuru dhidi ya bidhaa za China bila ya msingi wowote.

  Baadhi ya Wamarekani kuendelea kuishinikizia China kwa njia ya kuongeza ushuru kunatokana na kuupima uwezo wa China kimakosa wa kukabiliana na mgogoro huo. Kwa kweli, China ina uwezo wa kukabiliana na umwamba wa kibiashara wa Marekani kwa njia ya kupanua mahitaji ya ndani na mikakati anuai ya soko, pamoja na kuzidi kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango.

  Baadhi ya wamarekani wanajaribu kukanyaga kanuni za biashara ya pande nyingi, na kutekeleza umwamba wa kibiashara, watawaharibu maslahi ya wengine huku wakijiathiri vibaya. China inapenda kutafuta ufumbuzi wa masuala hayo kwa njia ya majadiliano na ushirikiano, na kupinga kithabiti kufanya vita vya biashara vipambe moto. Ikiwa Marekani inaendelea na hatua hizo, China italazimika kupambana hadi mwisho bila ya chaguo lingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako