Aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD) ,ambao alisema ni mchakato mzuri unaowakilisha nia ya matumaini na ushirkiano.
Alisema uvumbuzi wa TICAD umekuwa wastani na kwamba mkutano huo umeendelea kukua sanjari na vipaumbele vya Afrika.
Aliongeza kuwa mabadiliko makubwa ni umuhimu uliopatiwa sekta binafsi katika mkutano huo wa TICAD.
Aidha Rais Kagame aliitaja Rwanda kama mfano bora wa mafanikio wakati maendeleo ya sekta binafsi yanapowekwa katika mkakati wa ustawi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |