• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yasema maendeleo ya China katika miaka 70 yameitia moyo Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-29 19:55:00

    Wakati maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa China yanakaribia, maofisa waandamizi wa Uganda wamesema Bara la Afrika linaweza kuiga mfano wa maendeleo ya China yaliyopatikana katika miongo kadhaa iliyopita.

    Waziri wa nchi wa Uganda anayeshughulikia mambo ya nje Bw. Henry Okello Oryem, amesema China inaendelea kuchangia uzoefu wa maendeleo na nchi za Afrika wakati ikiwa kwenye hatua ya juu ya maendeleo yake ya viwanda.

    Amesema China na Afrika zinaendelea kuwa na uhusiano mzuri na wenye kunufaishana ambapo kila upande unautendea vizuri upande mwingine kwa usawa. Pia amesema katika miaka 30 ijayo Afrika itakuwa na maendeleo ya viwanda kutokana na msaada wa China.

    Bw. Oryem amesema Uganda inafanya mazungumzo na China kuhusu kurefusha reli ya SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi, ili ifike Uganda. Bw. Oryem pia amesema Uganda inashirikiana na China katika miradi minane mikubwa iliyopendekezwa na China na nchi kadhaa za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako