• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mhandisi aagizwa kuanisha maeneo yasiyo na maji wilaya ya Arumeru

  (GMT+08:00) 2019-08-29 20:01:01

  Naibu Waziri wa Wizara ya Maji Tanzania,Jumaa Aweso,amemwagiza mhandisi wa Mkoa wa Arusha,Joseph Makaidi,kuandaa andiko na kuainisha maeneo yasiyo na maji katika wialaya ya Arumeru.

  Lengo la andiko hilo ni kuwezesha kampuni ya Fraju Group Ltd inayokamilisha kazi ya ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya King'ori kwa gharama ya Sh.bilioni 1.5.

  Aweso alisema mkandarasi huyo amekuwa mfano wa kuigwa kwa kutekeleza mradi wake wa usambazaji maji katika kijiji cha King'ori unaotekelezwa chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini.

  Alisema mkandarasi huyo ametekeleza mradi huo kwa uaminifu na maji yaliyopo ni mengi mpaka yanapasua mabomba,hivyo lazima kumwongezea eneo la kusambaza maji hayo,badala ya kusambaza kijiji hicho pekee wakati wengine wanakosa maji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako