• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya fedha ya Marekani yasema haitaki kuingilia kiwango cha ubadilishaji wa sarafu cha dola ya kimarekani

    (GMT+08:00) 2019-08-29 20:08:19

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin amesema, hivi sasa wizara ya fedha ya nchi hiyo haitaki kuingilia soko la sarafu za kigeni, lakini hali hiyo inaweza kubadilika katika siku za baadaye. Pia amesema, kutokana na ukubwa na mzunguko wa soko la dola ya kimarekani, kama wizara hiyo ikitaka kuingilia soko hilo, njia nzuri zaidi ni hatua za ushirikiano.

    Kigezo cha dola za kimarekani ambacho kinalinganisha sarafu hiyo ya Marekani na sarafu nyingine sita kuu, kimeongezeka kwa kiasi kidogo baada ya waziri huyo kusema hivyo.

    Hivi karibuni rais Donald Trump wa Marekani ameeleza kwa mara kadhaa kutoridhishwa na dola ya kimarekani kuwa na nguvu, huku akisisitiza kuwa sarafu hiyo inaifanya Marekani kuwa na ugumu wa kushindana na nchi nyingine hata kumkosoa mkuu wa benki kuu ya nchi hiyo. Hoja hizo zimeleta wasiwasi kuhusu serikali ya Marekani kuweza kuingilia hali ya dola ya kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako