• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yafurahia kuona Afrika kupata wenzi wa ushirikiano wa aina tofauti

  (GMT+08:00) 2019-08-29 20:08:48

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China siku zote inafurahia kuona Afrika inakuwa na wenzi wa ushirikiano wa aina mbalimbali, huku akitaka mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya Afrika wa Tokyo TICAD uliofanyika nchini Japan uzingatie kihalisi ushirikiano na kuhimiza maendeleo ya Afrika.

  Habari zinasema mkutano wa saba wa TICAD hivi karibuni umefunguliwa huko Yokohama, Japan. Bw. Geng amesema kuunga mkono Afrika kutimiza amani na maendeleo kunalingana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa, na pia ni majukumu ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Nchi za Afrika zinatarajia mkutano wa TICAD kuwa jukwaa la ushirikiano wa pande nyingi linalofuatilia maendeleo ya Afrika na kutoa mchango katika upande huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako