• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania awataka viongozi wa zamani wa Afrika kulinda rasilimali

  (GMT+08:00) 2019-08-30 08:42:53

  Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliwataka viongozi wa zamani wa Afrika kuwa mstari mbele katika kulinda na kuendeleza rasilimali kubwa zilizopo barani Afrika kwa manufaa ya watu wake.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Magufuli ambaye alikuwa akiongea kwenye mkutano wa 6 wa Jukwaa la Viongozi wa Afrika uliofanyika ikulu, amewataka viongozi hao kuelewa kwamba rasilimali za Afrika zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wa uchumi. Amebainisha kuwa baada ya nchi za Afrika kupata uhuru wa kisiasa, malengo sasa yanapaswa kuelekezwa katika kujipatia uhuru wa kiuchumi kupitia usimamizi mzuri wa rasilimali, hasa mali asili.

  Mkutano huo uliojadili changamoto zinazolikabili bara la Afrika umewakutanisha marais wa zamani wa Tanzania, Afrika Kusini, Somalia na Madagascar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako