Jamii ya wafanyabiashara wa Uingereza jana imeendelea kuwa na wasiwasi juu ya mgogoro wa kisiasa huku vita vya maneno juu ya uamuzi wa waziri mkuu Boris Johnson wa kusimamisha bunge la Uingereza vikizidi kupamba moto.
Mkurugenzi Mkuu wa shirikisho la wafanya biashara BCC Adama Marshal amesema biashara nchini Uingereza imekuwa kwenye mchezo usiokwisha wa chesi ya kisiasa, wakati biashara kadhaa na hali ya uchumi ya Uingereza ikiwa hatarini.
Johnson amepata idhini kutoka kwa Malkia Elizabeth ya kusimamisha bunge, au kuahirisha kwa karibu wiki tano katika mwezi Septemba na Oktoba. Wakosoaji wanasema hatua hiyo inaaminiwa kuwa ni jaribio la Johnson kupunguza nafasi za wabunge kupitisha sheria za kuzuia Brexit bila ya makubaliano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |