• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu na watunga sera wa Afrika watoa mwito wa kubadilisha mwelekeo wa sasa wa kutekeleza makubaliano ya hali ya hewa ya Paris

  (GMT+08:00) 2019-08-30 08:59:36

  Wataalamu na watunga sera wa Afrika wametoa wito wa kubadilisha "njia dhaifu" katika utekelezaji wa Makubaliano ya Paris ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

  Wito huo umetolewa kwenye Mkutano wa 8 kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maendeleo barani Afrika unaoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Agosti 28 hadi 30.

  Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa, Benki ya maendeleo ya Afrika na Shirika linalojihusisha na masuala ya hali ya hewa PACJA, ulifunguliwa kwa wito mkubwa kutoka kwa mawaziri na wataalamu wa Afrika wa kubadilisha njia ya sasa isiyosisimua ya kutelekeza Makubaliano ya Paris.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako