• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa pili wa Ebola wathibitishwa magharibi mwa Uganda

    (GMT+08:00) 2019-08-30 09:15:40

    Wizara ya afya ya Uganda jana ilitangaza mlipuko wa pili wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Kasese, kilomita 472 kutoka mji mkuu wa Kampala, baada ya mgonjwa mmoja wa Ebola kuingia nchini humo kutoka nchi jirani DRC.

    Kwenye taarifa yake waziri wa afya wa nchi hiyo Joyce Moriku Kaducu amesema, msichana mmoja Mkongo mwenye umri wa miaka 9 aliyeingia Uganda pamoja na mamake Jumatano kupitia mpaka wa Mpondwe kutafuta huduma za matibabu katika hospitali ya Bwera, amethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola.

    Amesema kuwa, mtoto huyu aligunduliwa kuwa na homa kali, kukosa nguvu mwilini, vipele na kutokwa na damu mdomoni.

    Ameongeza kuwa, tangu mgonjwa huyu agunduliwe katika eneo la kuingia Uganda hajafanya mawasiliano yoyote nchini humo. Kwa sasa mtoto huyu anasimamiwa katika kituo cha matibabu ya Ebola cha Bwera, Kasese.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako