• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Virgil van Dijk awabwaga Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, achukua tuzo mbili

  (GMT+08:00) 2019-08-30 09:22:29

  Beki wa majogoo wa Anfield Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk amewaangusha wazoefu wa soka duniani Christian Ronaldo na Lionel Messi kwenye tuzo za wanasoka bora wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) usiku wa jana mjini Monaco.

  Van Dijk amenyakua tuzo mbili ya mchezaji bora na beki bora wa kiume wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita.

  Takwimu za michezo ya mwaka 2018-19 zinaonesha kuwa, Van Dijk aliiwakilisha klabu na taifa lake katika mechi 59. Alifunga mabao tisa na kusaidia ufungaji wa mabao manne. Pia alichezea Liverpool kwa dakika 4,465 ambazo ni nyingi zaidi ya mchezaji mwingine yeyote. Katika mashindano yote ameonesha kwa zaidi ya 70% umuhimu wake kama beki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako