• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi ya Mabingwa Ulaya- Makundi yatajwa-kwa mara nyingine Samatta uso kwa uso na Mane

    (GMT+08:00) 2019-08-30 09:21:43
    Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji anayochezea nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi E ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na bingwa mtetezi Liverpool ya Uingereza, Napoli ya Italia na Salzburg ya Austria.

    Katika droo hiyo iliyofanyika sambamba na tuzo za mwanasoka bora wa Ulaya, Mbwana Samatta amejikuta timu yake ya KRC Genk ikipangwa kundi moja na Liverpool ambapo Sadio Mane raia wa Senegal watakutana kwa mara nyingine.

    Mane aliiongoza Senegal kuichapa Tanzania ya Samatta 2-0 kwenye mechi ya Kundi C fainali za kombe la mataifa ya Afrika Juni mwaka huu nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako