Watu 15,192 wameambukizwa Chikungunya baada ya ugonjwa huu kulipuka katika mji wa mashariki wa Ethiopia Dire Dawa. Ugonjwa huo unaoambukizwa kwa mbu, ni nadra kutishia maisha, na hupona wenyewe ndani ya siku mbili tatu. Mkurugenzi wa muda wa taasisi ya afya ya umma ya nchi hiyo Mesfin Wossen amesema hadi sasa hakuna kifo kilichoripotiwa, na sababu moja ni kwamba wagonjwa wamepata matibabu kwa wakati. Amewataka watu kusaidia kupuliza dawa ya mbu kwenye maeneo yenye tishio la Chikungunya mjini Dire Dawa, kuondoa maji yoyote ya mvua yaliyotuwama, na kufunika vitu vyote vya maji kwa vitambaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |