• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya TMEIC ya Japan yaona sera ya China ya kupunguza kodi inatia moyo makampuni ya kigeni kuhusu soko la China

    (GMT+08:00) 2019-08-30 17:04:09

    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imekuwa inatekeleza hatua mbalimbali za kupunguza kodi, na kuziletea kampuni za kigeni faida kubwa zaidi. Mkuu wa Kampuni ya umeme ya Toshiba Mitsubishi ya Japan amesema, sera hizo za China zimeongeza imani ya kampuni hiyo kuhusu soko la China, na kutoa msukumo mpya kwa maendeleo yake nchini China.

    VAT ni kodi muhimu inayotozwa na serikali ya China. Ili kuandaa mazingira mazuri zaidi kwa makampuni, serikali ya China ilipunguza kiwango cha VAT kutoka asilimia 17 hadi asilimia 16 dhidi ya viwanda vya uzalishaji kuanzia mwezi Mei mwaka jana, na kuzidi kuipunguza hadi asilimia 13 mwezi Aprili. Meneja mkuu wa Kampuni ya Toshiba Mitsubishi ya Japan nchini China Bw. Ma Qun akizungumzia faida zinazopatikana kutokana na upunguzaji wa kodi hii anasema:

    "Hadi sasa sera hii imeisaidia kampuni yetu kupunguziwa kodi ya Yuan milioni 2 tangu ilipoanza kutekelezwa."

    Takwimu zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza mwaka huu, China imepunguza kodi yenye thamani ya RMB yuan trilioni 1.2. Naibu meneja mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Liu Jifeng anaona kupunguzwa kwa kodi pia kutachangia kuongeza uhai wa soko. Anasema:

    "Sera hii ya kupunguza kodi vilevile itachangia soko, kwani inahimiza mahitaji ya soko, kwa upande mwingine soko litahimiza maendeleo ya viwanda vya uzalishaji, ambao utakuwa mzunguko mzuri."

    Wataalamu wameeleza kuwa, utekelezaji wa sera ya kupunguza kodi umepunguza mzigo kwa makampuni, na kutoa mchango mkubwa kwa katika kuongeza imani ya makampuni, kutuliza makadirio ya soko, na kuhimiza uchumi kuendeshwa kwa utulivu. Mbali na hayo, sera hii imeongeza mvuto wa mazingira ya biashara ya China kwa wawekezaji wa kigeni.

    Takwimu kutoka Wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, thamani ya matumizi ya fedha ya China kati mwezi Januari hadi Julai ilikuwa RMB yuan milioni 53, likiwa ni ongezeko la asilimia 7.3. Bw. Liu Jifeng ameeleza kuwa, sera ya kupunguza kodi itayapa imani zaidi makampuni ya kigeni kuhusu soko la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako