• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanaoivuruga Hong Kong wakamatwa kutokana na tuhuma kadhaa

  (GMT+08:00) 2019-08-30 18:49:39

  Polisi wa Hong Kong wamethibitisha kuwa watu wanaovuruga Hong Kong Joshua Wong na Agnes Chow, leo asubuhi wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Aberdeen na Tai Po, huku mwingine anayeitwa Andy Chan akikamatwa jana usiku wakati akipita forodha ya uwanja wa ndege wa Hong Kong. Watu hao watatu wanakabiliwa na mashtaka kadhaa.

  Kutokana na waandamanaji walizingira makao makuu ya polisi Juni 21, polisi wa Hong Kong walifanya uchunguzi wa kina na kufanya operesheni leo kumkamata Joshua Wong mwenye umri wa miaka 22 huko Aberdeen. Kwa mujibu wa polisi, Joshua Wong anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwachochea wengine kushiriki kwenye mkusanyiko usioidhinishwa, kuandaa mkusanyiko usioidhinishwa na kushiriki kwenye mkusanyiko usioidhinishwa huku akifahamu.

  Polisi siku hiyo pia wamemkamata Agnes Chow mwenye umri wa miaka 22. Imefahamika kwamba Agnes Chow ana tuhuma mbili za kuwachochea wengine kushiriki kwenye mkusanyiko usioidhinishwa na kushiriki kwenye mkusanyiko usioidhinishwa huku akifahamu.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, Andy Chan alikamatwa kutokana tuhuma za kuwajeruhi watu wengine wakati akiondoka Hong Kong kuelekea Tokyo, Japan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako