• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu waitaka Kenya kupanua wigo wa kodi kwa kuilenga sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2019-08-30 19:47:20

    Wataalamu wameitaka Kenya kupanua wigo wake wa kodi kwa kuilenga sekta binafsi ya uchumi.

    Mwenyekiti wa taasisi ya wahasibu wa umma wa Kenya kwa ajili ya kituo cha bodi ya fedha za umma na kodi Bw. Philip Muema, kwenye kongamano mjini Nairobi kuwa Kenya inashindwa kufikia malengo yake ya kifedha kutokana na kuwa sehemu kubwa ya watu wake wako nje ya wigo wa kodi.

    Amesema bado serikali ya Kenya haijawa na muundo wa kodi unaoweza kutambua mapato kutoka kwa sekta binafsi, ambayo inatoa fursa kubwa ya ajira nchini Kenya. Amesema mpaka sasa wigo wa kodi nchini Kenya unawafikia watu milioni 5.7 kwenye nchi yenye watu wanaokadiriwa kuwa milioni 45.

    Mkurugenzi wa mambo ya taaluma katika Taasisi ya mambo ya umma ya na utawala ya Strathmore Bw. Thomas Kibua, amesema serikali inaweza kuongeza mapato ya kodi kupitia kutoa huduma za msingi kwa umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako