• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SAA yatozwa faini kwa kuwaingiza wakimbizi Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-08-30 19:56:53
    Idara ya mambo ya ndani ya Afrika Kusini imelitoza faini shirika la ndege la Afrika kusini Randi milioni 4 katika mwaka wa fedha wa 2017-2018 kwa kuwaingiza nchini humo wakimbizi wasiokuwa na vibali rasmi vya kukaa nchini humo.Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bw Aaron Motsoeledi amesema waliamua kuchukua hatua hiyo ili iwe funzo kwa shirika hilo na mashirika mengine ya kutoa huduma za usafiri nchini humo.Shirika hilo ni miongoni mwa mashirika saba ambayo yametozwa faini kwa kuwaingiza wakimbizi nchini humo bila vibali rasmi.Mashirika mengine ya ndege ambayo yametozwa faini ni pamoja na mashirika ya Emirates, Kenya Airways, British Airways miongoni mwa mengine.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako