• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la wafanyabiashara la Marekani laonya ongezeko la mgogoro wa kibiashara linaweza kusababisha kushuka kwa uchumi wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-30 20:02:50

    Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara la Marekani Bw. Thomas J. Donohue ameonya kwamba ongezeko la mgogoro wa kibiashara linaweza kusababisha kushuka kwa uchumi wa Marekani, na ametoa wito wa kuanza tena mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

    Makala ya Bw. Donohue iliyochapishwa kwenye tovuti ya Washington Post imeeleza kuwa uwekezaji wa kampuni za Marekani umeanguka kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu iliyopita kutokana na kupamba moto kwa mgogoro wa kibiashara na ukuaji dhaifu wa uchumi wa dunia, na wakati huo huo, uzalishaji viwandani wa Marekani pia umepungua tangu Desemba mwaka jana, mapato ya kilimo yameanguka sana, na kiashiria cha hatari kilichoonekana kwenye soko la hisa la Marekani kwa mwezi huu kimesababisha wawekezaji kuwa na hofu, na kwa mujibu wa historia hii ni dalili ya kudorora kwa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako