• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya inapanga kuitisha mkutano wa Afrika kujadili usalama wa chakula

    (GMT+08:00) 2019-08-30 20:12:15

    Wiki ijayo Kenya itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Afrika nzima kujadili mikakati mipya yenye lengo la kuhimiza usalama wa chakula barani Afrika na matishio ya afya ya binadamu.

    Katibu mkuu wa wizara ya kilimo ya Kenya Bw. Mwangu Kiunjuri amesema serikali na mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shirika la afya duniani (WHO) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) wanashirikiana kuandaa mkutano huo utakaofanyika kati ya tarehe 2- 6 mwezi ujao, ili kuleta mwamko kuhusu usalama wa chakula Afrika.

    Bw. Kiujuri amesema masuala ya usalama wa chakula ni kipaumbele kwa nchi nyingi za Afrika, na Kenya inaona fahari kuwa na fursa ya kuandaa mkutano huo na kuchangia mawazo na njia za kubadilishana bidhaa, ili kuweka vigezo vinavyofaa kwa eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako