• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 10 wapigwa risasi na kujeruhiwa katika mechi ya soka ya shule ya sekondari jimboni Alabama nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-31 17:26:31

    Takriban watu 10 wenye umri kati ya miaka 15 na 18 wamepigwa risasi na kujeruhiwa katika mechi ya soka ya shule ya sekondari huko jimboni Alabama nchini Marekani.

    Ufyatuaji risasi huo ulitokea jana jioni muda mfupi tu baada ya timu mbili za shule ya sekondari kumaliza mechi kwenye uwanja wa michezo uliopo mji wa Mobile. Wafanyakazi wa zima moto wamethibitisha kuwa watu hao 10 walipelekewa hospitali, ambapo watano kati yao wakiwa wameumia sana lakini hawakuwa mahututi. Polisi ya huko imesema kwa sasa watu wawili wanashikiliwa baada ya tukio hilo lakini bado hawajathibitishwa kuwa ni watuhumiwa.

    Mkuu wa polisi wa mji wa Mobile Lawrence Battiste amelaani matumizi ya bunduki na kuleta vurugu kwenye michezo, akisema wanapeleka ugomvi wao kwenye michezo na kuwaweka watu wengine hatarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako