• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Hong Kong walaani shambulizi la kisu dhidi ya afisa aliye kuwa akitoka kazini

  (GMT+08:00) 2019-08-31 17:33:44

  Kamshina wa polisi wa Hong Kong Lo Wai-chung amelaani vikali shambulizi la kisu dhidi ya ofisa mmoja aliye kuwa akitoka kazini na kuahidi kufanya uchunguzi kamili juu ya tukio hili.

  Akimtembelea ofisa huyo, ameeleza kusikitishwa kwake na kusema shambulizi la kikatili kama hilo ni la kuaibisha, ameongeza kuwa kumjeruhi mtu makusudi ni uhalifu mkubwa sana ambao unaweza kupelekea kifungo cha maisha gerezani.

  Ofisa mwenye umri wa miaka 45 alishambuliwa na wanaume watatu kwa kisu alipokuwa akitembea kwa miguu kwenye barabara ya Kwai Yi saa 5:15 usiku siku ya Ijumaa na kujeruhiwa mkononi na begani.

  Vyombo vikuu vya habari na sekta mbambali za jamii mkoani Hong Kong leo zimesema kwa kuwakamata wahalifu wa vurugu, polisi wanatenda haki na kuwapa onyo wapangaji wa machafuko yanayoendelea mkoani Hong Kong wasimamishe shughuli zao mbaya mara moja.

  Polisi wa Hong Kong jana walithibitisha kuwa wamewakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kushiriki kwenye vuguru za kimabavu na kuharibu vifaa vya umma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako