• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakanusha kauli za baadhi ya wanasiasa wa Marekani kuhusu Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-08-31 18:27:47

  Ofisi ya Kamishna ya wizara ya mambo ya nje ya China katika Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong, imeeleza kutoridhishwa na kupinga vikali kauli za baadhi ya wanasiasa wa Marekani.

  Inaripotiwa kuwa Kiongozi wa wabunge wenye viti vichache wa Baraza la Seneti Chuck Schumer, mwakilishi Jim McGovern na afisa wa ikulu wamewakosoa polisi wa Hong Kong kwa kuwakamata watu wanaoleta vurugu, wakiwatetea kuwa wao ni wapinzani tu, na kuitaka serikali ya Hong Kong kuwafutia mashtaka mara moja na kutishia kwa mswada.

  Akijibu kauli hizo, msemaji wa ofisi hiyo amesema wanasiasa hao wamevuruga ukweli, kuwatetea wakosaji, kuingilia kwa uwazi mambo ya Hong Kong, ambayo ni mambo ya ndani ya China, na tena kubainisha unafiki wao, mawazo ya umwamba na upendeleo wa wanasiasa wa Marekani. Na kusisitiza kuwa kauli kama hizo wanazibeza na kuzikanusha vikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako