• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yamkosoa mwanasiasa wa EU kwa kuwa na wasiwasi wa kinafiki

  (GMT+08:00) 2019-08-31 18:28:16

  Ofisi ya Kamishna wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong, imeeleza kutokubaliana na kuwapinga vikali baadhi ya maofisa wa Umoja wa Ulaya kuingilia kwa uwazi mambo ya Hong Kong, ambayo ni mambo ya ndani ya China.

  Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi hiyo, polisi wa Hong Kong wameeleza bayana sababu za kuwakamata watu wanaoleta vurugu, ambazo ni za msingi, zinazofuata sheria na zisizoweza kupingika. Amesisitiza kuwa kwa kuvuruga ukweli na kueleza wasiwasi wao, wanasiasa wanaohusika wa Umoja huo wamejaribu kuzuia juhudi za utekelezaji wa kawaida wa sheria na kuvuruga utawala wa sheria wa Hong Kong.

  Msemaji huyo amesema hayo akijibu kauli ya hivi karibuni ya mwalikishi mkuu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulika na masuala ya kigeni na sera ya usalama Federica Mogherini, kwamba maendeleo huko Hong Kong, hasa katika saa hizi za mwisho, yanatia wasiwasi sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako