• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Barabara inayojengwa na kampuni ya China kubadilisha maisha ya jamii za Kenya

  (GMT+08:00) 2019-09-01 17:09:40

  Barabara muhimu inayounganisha Kenya na Sudan Kusini ambayo imekuwa ikiendelea kujengwa na Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi ya Teknolojia ya Anga ya China kwa gharama za shilingi bilioni 2 za Kenya inatarajiwa kubadilisha jamii za huko kupitia usafiri wa haraka na biashara.

  Katika ziara yake ya ukaguzi wa barabara ya Kitale hadi Chepchoina iliyofanyika jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Barabara ya Kenya Lukas Kimeli amesema barabara hiyo italeta mabadiliko makubwa kwenye uchumi wa kaunti za kaskazini magharibi mwa Kenya itakapomalizika Julai mwaka 2021. Ofisa huyo pia ameeleza kuridhishwa na kazi ya kampuni hiyo na kuwahakikishia wakazi kwamba barabara itakamilika ndani ya muda uliopangwa na kuleta faida nyingi za kiuchumi kwa jamii za huko.

  Madereva wa magari wanaoendesha kwenye barabara inayosafiri kwenye kaunti kadhaa za kaskazini magharibi za Kenya wameanza kuishukuru kampuni ya China kwa kuiendeleza barabara hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako