• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hong Kong yalaani vikali vitendo haramu na vya kimabavu vya waandamanaji wenye msimamo mkali

  (GMT+08:00) 2019-09-01 17:15:12

  Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong imelaani vikali vitendo haramu na vya kimabavu vya waandamanaji wenye msimamo mkali vinavyozidi kuongezeka bila ya kujali usalama wa umma.

  Akikumbusha taarifa ya pingamizi iliyotolewa na polisi, msemaji wa serikali ya Hong Kong ametoa taarifa kuwa mikusanyiko isiyoidhinishwa na maandamano yaliyofanyika jana katika sehemu mbalimbali yalizuia vibaya barabara na kuvuruga usafiri kisiwani Hong Kong na kuathiri vibaya huduma za dharura na maisha ya watu. Taarifa hiyo pia imesema waandamanaji wenye msimamo mkali walikabiliana na polisi katika maeneo mbalimbali na kurusha mabomu mengi ya petroli dhidi ya majengo ya serikali, jengo la Bunge, makao makuu ya polisi pamoja na sehemu nyingine, na kuwashambulia maofisa wa polisi kwa maji babuzi na matofali. Vilevile, waandamanaji hao walichoma moto katika sehemu mbalimbali, kuharibu mali za umma, kuweka vizuizi na kuharibu vifaa katika vituo vya reli ya chini ya ardhi.

  Leo alfajiri saa chache baada ya waandamanaji hao kufanya vitendo hivyo viovu, msemaji wa jeshi la polisi la Hong Kong Bibi Yu Hoi-klwan alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa Hong Kong ilishuhudia maafa makubwa jana usiku na watu zaidi ya 40 wamekamatwa na polisi kutokana na vitendo vyao vya kukiuka sheria. Pia amekiri kuwa maofisa wawili wa polisi walifyatua risasi mbili angani kama onyo jana katika Bustani ya Victoria wakati walipozingirwa na kushambuliwa na waleta fujo hao huku maisha yao yakiwa hatarini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako