• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu Uingereza- Arsenal wapunguzwa kasi, Everton kumekucha

    (GMT+08:00) 2019-09-02 08:49:12
    Washika bunduki wa London Arsenal imelazimisha sare ya mabao 2-2 na Tottenham Hotspurs kwenye uwanja wa Emirates. Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali, Spurs watajilaumu wenyewe baada ya kuongoza kwa mabao mawili kabla ya wenyeji Arsenal kusawazisha.

    Spurs ilipata bao lake la kwanza kupitia Christian Eriksen baada ya kipa wa Arsenal, Bernd Leno kushindwa kuokoa mpira. Mshambuliaji Harry Kane alifunga bao la pili la Spurs kwa mkwaju wa penalti baada ya Granit Xhaka kumchezea vibaya Son Heung-min katika eneo la hatari.

    Arsenal ilipata bao lake la kwanza kabla ya mapumziko kwa Alexandre Lacazette aliyewatoka mabeki wa Spurs na kupiga shuti lililomshinda kipa Lloris na kujaa nyavuni.

    Dakika 20 kalba mpira kumalizika, mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang aliisawazishia Arsenal akiunganisha shuti lililopigwa na Guendouzi.

    Mchezo mwingine ulikuwa baina ya Everton iliyowachabanga Wolverhampton kwa magoli 3-2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako