• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 159 wakamatwa kwa kufanya vurugu wikiendi iliyopita huko Hong Kong

    (GMT+08:00) 2019-09-02 19:12:02

    Polisi katika Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong wamewakamata watu 159 wanaotuhumiwa kufanya vurugu kubwa wikiendi iliyopita.

    Akiongea na wanahabari Mrakibu Mkuu wa Tawi la Polisi la Uhusiano wa Umma Tse Chun-chung amesema kuwa watu waliokamatwa wakiwemo wanaume 132 na wanawake 27, wenye umri kati ya miaka 13 na 58, wanatuhumiwa kufanya mikusanyiko kinyume na sheria, kumiliki silaha hatari na kuwashambulia na kuwazuia polisi. Amesema watuhumiwa wengine wanane wamekamatwa leo asubuhi kwa makosa ya kumiliki silaha hatari na kukiuka amri ya mahakama baada ya waandamanaji wenye msimamo mkali kuvunja operesheni katika vituo tofauti vya MTR.

    Wakati huohuo mkurugenzi wa idara ya usalama ya mkoa wa Hong Kong Lee Ka-chiu amesema waandamanaji wenye hasira wamewashambulia na kuwapiga watu wenye mtazamo tofauti na kuzua hofu katika jamii. Amefafanua kuwa katika siku mbili zilizopita, waandamanaji hao wamesababisha uharibifu, na kusema kuongezeka na kupanuka kwa vurugu hizo kumedhoofisha operesheni, kanuni na utawala wa sheria wa Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako