• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washauri bingwa wa Zambia kufanya tathmini ili kupata fursa zaidi za Ukanda Mmoja, Njia Moja

    (GMT+08:00) 2019-09-03 08:24:43

    Washauri bingwa wa Zambia wamesema wanakusudia kufanya tathmini juu ya nchi hiyo ilivyofanya hadi sasa katika kunufaika na fursa zinazotokana na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Uangalizi wa Sera, Bernadette Deka-Zulu amesema washauri bingwa watashirikiana na washirika wengine kufanya tathmini hiyo ambayo itahusisha ufuatiliaji na kutathmini wizara maalumu juu ya miradi iliyofanya kuhusiana na pendekezo hilo na kama miradi hiyo imezaa matunda mazuri.

    Kulingana na Bi. Deka-Zulu, China imeonesha nia na utayari kwenye mchakato wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kwamba ni juu ya nchi washirika kushiriki kwenye pendekezo na kuja na miradi itakayoleta manufaa yanayohitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako