• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Kusini yaupongeza Umoja wa Afrika kwa kuharakisha ujenzi wa kambi za wanajeshi

  (GMT+08:00) 2019-09-03 08:25:02

  Sudan Kusini jana ilikaribisha shehena ya mahema yaliyopelekwa nchini humo na Kamati ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika ili kusaidia ujenzi wa kambi za wanajeshi nchini humo.

  Wizara ya mambo ya nje imeupongeza Umoja wa Afrika kwa uungaji mkono wake ambao utaleta wepesi kwenye kambi zinazocheleweshwa za serikali na vikosi vya waasi, kufuatia wasiwasi kwamba pande mbili zenye mzozo zinaweza kushindwa kumaliza masuala yaliyopo ndani ya miezi mitatu iliyosalia ya kipindi kilichoongezwa cha mpito.

  Wiki iliyopita Sudan Kusini ilipokea shehena ya mahema 640 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ambayo yatagawanywa kwenye maeneo 35 ya kambi nchi nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako