• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaishtaki Marekani katika WTO

    (GMT+08:00) 2019-09-03 08:55:28

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China amesema, Septemba 1 Marekani imetekeleza rasmi hatua ya kuongeza ushuru wa asilimia 15 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 za kimarekani zinazouzwa nchini Marekani, hivyo China imeishtaki Marekani chini ya mfumo wa utatuzi wa migongano wa Shirika la biashara duniani WTO.

    Ameongeza kuwa hatua hiyo ya Marekani imekiuka vibaya makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili huko Osaka, na China inaipinga vikali hatua hiyo. China italinda kithabiti maslahi yake halali na kulinda mfumo wa biashara za pande nyingi na utaratibu wa biashara za kimataifa kutokana na kanuni husika za shirika la WTO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako