• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaonya juu ya kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula

    (GMT+08:00) 2019-09-03 09:02:30

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD jana limeonya juu ya kuzorota kwa hali ya usalama wa chakula kutokana na ukosefu wa mvua, migogoro na msukosuko wa kiuchumi.

    Shirika hilo limesema, Ethiopia, Sudan na Sudan Kusini zinatarajiwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoathirika na msukosuko wa chakula duniani.

    Ripoti ya kila mwaka ya kimataifa kuhusu msukosuko wa chakula inaonyesha kuwa, watu karibu milioni 27, ambao ni sawa na asilimia 24 ya watu wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula chakula duniani, wanaishi katika nchi 7 kati ya nane za IGAD mwaka 2018.

    Habari nyingine kutoka Kitengo cha usalama wa chakula na uchambuzi wa lishe FSNAU, kilichopo chini ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO zinasema, watu karibu milioni 2.1 nchini Somalia wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula hadi mwezi Desemba kutokana na ukame.

    Matokeo ya tathimini yaliyotolewa na kitengo hicho yanaonesha kuwa watoto karibu milioni 1 chini ya miaka 5 huenda watakuwa na utapiamlo ifikapo katikati ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako