• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania awahimiza viongozi wa asasi za kiraia kuunga mkono ajenda ya mageuzi

  (GMT+08:00) 2019-09-03 09:34:18

  Rais John Magufuli wa Tanzania amewahimiza viongozi wa asasi za kiraia kuunga mkono ajenda yake ya mageuzi inayolenga kustawisha nchi.

  Akizungumza kwenye mkutano na viongozi wa asasi za kiraia katika Ikulu jijini Dar es Salaam, rais Magufuli amesema ameanza kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa inayolenga kuiwezesha nchi yake kufikia lengo la kuwa nchi yenye kipato cha kati kabla ya mwaka 2025, tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

  Rais Magufuli amewaambia viongozi wa asasi hizo kuwa ni wajibu wao kuhakikisha nchi hiyo inadumisha usalama na ustawi.

  Hata hivyo, rais Magufuli amewatahadharisha dhidi ya kujihusisha na mienendo inayokiuka maadili, akisema kufanya hivyo si kama tu kunaharibu sifa zao binafsi bali pia sifa ya taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako