• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yazindua Wiki ya kwanza ya Filamu ya China kuongeza ushirikiano wa kiutamaduni

  (GMT+08:00) 2019-09-03 09:44:15

  Waziri wa Mawasiliano ya Habari na Teknolojia wa Kenya Bw. Joe Mucheru amesema kuwa Wiki ya Filamu ya China ambayo ni ya kwanza na ya aina yake nchini humo inafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 mwezi huu ili kuongeza ushirikiano wa kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili. Wakenya watatazama filamu maarufu 10 za Kichina bila malipo. Katika wiki hiyo zitaonyeshwa filamu za China za aina tofauti, kama vile mapigano, ucheshi, mapenzi na maisha ya kawaida.

  Mshauri wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema Wiki ya Filamu ya China mjini Nairobi ni mojawapo ya shughuli za kuadhimisha miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako