• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kufuzu Kombe la Dunia 2022- Burundi uso kwa uso na Tanzania, Ndayiragije awataka Warundi wamsamehe, asema yupo kazini

  (GMT+08:00) 2019-09-03 10:31:13
  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Etienne Ndayiragije amewaambia Warundi kuwa yupo kazini hivyo wasitarajie huruma yoyote kutoka kwake, Ndayiragije ni raia wa Burundi anatarajiwa kuiongoza Taifa Stars dhidi ya taifa lake la Burundi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar mwaka 2022.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ndariragije amesema kwa sasa yupo kazini na malengo yake ni kupata ushindi.

  Tanzania iko nchini Burundi tayari kwa mchezo wake wa kwanza utakaopigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Prince Louis Rwagasore jijini Bujumbura na marudiano yatakuwa Septemba 8 jijini Dar es Salaam.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako