• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lukaku ashutumu tabia ya ubaguzi dhidi ya wachezaji weusi

  (GMT+08:00) 2019-09-03 10:31:52
  Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku anadai kuwa sasa mpira unarudishwa nyuma na ubaguzi. Amebainisha hayo mara baada ya mashabiki wa klabu ya Cagliari kumtukana wakati akichezea timu ya Inter Milan siku ya jumapili.

  Tukio limetokea mara baada ya wachezaji wa Manchester United Paul Pogba na Marcus Rashford pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham kutolewa lugha za kibaguzi kwenye mitandao ya kijamii.

  Klabu ambayo mashabiki wake walitoa kauli ya kibaguzi imetoa tamko la kukemea tabia hiyo na kusema kuwa wanamuunga mkono Lukaku na kudai kuahidi kupiga marufuku na kumchukulia hatua kali yeyote atakayehamasisha tabia hiyo ya ubaguzi kwa sababu ni kinyume kabisa na miiko ya klabu yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako