Ofisi ya habari ya Baraza la serikali ya China leo imetoa waraka maalumu kuhusu usalama wa nyuklia wa China, ambao ni wa kwanza kutolewa na serikali ya China kuhusu suala hilo.
Waraka huo umefafanua maendeleo ya mambo ya usalama wa nyuklia ya China, kanuni ya kimsingi na sera za China kuhusu usalama wa nyuklia, kueleza dhana na uzoefu wa China katika usimamizi wa usalama wa nyuklia, na kusisitiza dhamira na hatua zinazochukuliwa na China katika kuhimiza mchakato wa usimamizi wa usalama wa nyuklia duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |