• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa waraka wa kwanza wa usalama wa nyukilia

  (GMT+08:00) 2019-09-03 18:10:29

  Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China leo imetoa waraka wa kwanza wa "Usalama wa Nyukilia nchini China". Waraka huo unasema China imepitisha nyaraka zote za kimataifa kuhusu usalama wa nyukilia, na kuunga mkono juhudi za pande nyingi za kuimarisha usalama huo. Pia itaendelea kuhimiza ushirikiano wa kimataifa, na ujenzi wa mfumo wa kimataifa wa usalama wa nyukilia.

  Waraka huo unasema, China siku zote inachukulia suala la usalama wa nyukilia kama ni jukumu muhimu la kitaifa, na kufanikiwa kudumisha usalama huo kwa muda mrefu. Naibu waziri wa mazingira wa China, ambaye pia ni mkuu wa idara kuu ya usalama wa nyukilia Bw. Liu Hua anasema,

  "Hadi mwishoni mwa Juni mwaka huu, katika China bara kuna vinu 47 vya nyukilia vya kuzalisha umeme, vinu 19 vya nyukilia vya utafiti, vinu 18 vya kurudia kwa nishati ya nyukilia, na viwanda viwili vya kushughulikia taka za kinyukilia. Vinu na viwanda hivyo vyote vimedumisha rekodi nzuri ya usalama."

  Mwaka 2016, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA lilifanya tathmini kuhusu mfumo wa usimamizi wa usalama wa nyukilia, na kupata hitimisho kwamba, ufanisi wa usimamizi wa China kwa usalama wa nyukilia unaongezeka mfululizo, na mamlaka ya kusimamia usalama huo ya China inaaminika.

  Waraka huo pia unasema, China inatilia maanani mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi tofauti kuhusu usalama wa nyukilia, na imesaini zaidi ya makubaliano 50 ya kuhimiza ushirikiano na nchi mbalimbali, zikiwemo Ufaransa, Marekani, Russia, Japan, Korea Kusini na nchi nyingine zilizojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Bw. Liu amesema China pia imetoa jukwaa la kufanya mafunzo na mawasiliano kuhusu suala la nyukilia kati ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza dunia kuinua kiwango cha usalama wa nyukilia. Anasema,

  "China imeshiriki na kutekeleza nyaraka za kimataifa kwa hatua madhubuti, na imejiunga na karibu makualibano yote ya kimataifa yaliyotolewa na IAEA na Umoja wa Mataifa. China inaunga mkono kazi ya IAEA, na imekuwa nchi ya pili duniani inayochangia zaidi bajeti yake. China pia itaendelea kutoa fedha kwa mifuko ya usalama wa nyukilia, ili kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa nyukilia barani Asia, na kuhimiza kuinua kiwango cha usalama huo katika nchi tofauti duniani kwa uwiano."

  Aidha, waraka huo unasisitiza kuwa, China itaendelea kuhimiza ushirikiano wa kimataifa, na kuhimiza kujenga mfumo wa kimataifa wa usalama wa nyukilia wenye usawa, ushirikiano na mafanikio ya pamoja, ili kuziwezesha nchi zote duniani zinufaike na nishati ya nyukilia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako