• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakana kuwa chanzo kikuu cha Fentanyl nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2019-09-03 18:11:48

    Ofisi kuu inayopambana na dawa za kulevya ya China leo imetangaza kuwa, tangu China ianze kuweka dawa ya Fentanyl chini ya usimamizi wa serikali tarehe mosi Mei, haijagundua uhalifu wa magendo ya dawa hiyo. Naibu mkurugenzi wa tume ya kitaifa ya kupambana na dawa za kulevya ya China Bw. Liu Yuejin amesisitiza kuwa, China si chanzo kikuu cha dawa ya Fentanyl nchini Marekani.

    Kwenye mkutano na wanahabari, ofisi kuu inayopambana na dawa za kulevya ya China imeeleza hatua za China za kusimamia dawa ya Fentanyl. Naibu mkurugenzi wa tume ya kitaifa inayopambana na dawa za kulevya ya China Bw. Liu Yuejin anasema,

    "Tumekagua kwa kina viwanda vya kuzalisha dawa na vitu vya kikemikali, ili kuondoa uwezekano wa kutengeneza dawa ya Fentanyl. Pia tumefunga njia ya kuuza na kununua dawa hiyo kwenye mtandao wa Internet. Mbali na hayo, mamlaka ya usimamizi wa dawa pia inafanya ukaguzi maalumu kwa uzalishaji na mauzo halali ya dawa hiyo."

    Ili kukinga magendo ya dawa ya Fentanyl kutoka China kwenda nchi za nje, China imeshirikisha ofisi kuu inayopambana na dawa za kulevya, wizara ya usalama wa umma, idara kuu ya forodha na idara kuu ya posta kwenye operesheni ya miezi mitatu na nusu ya kupambana na magendo ya dawa hiyo.

    Hivi karibuni Marekani imeilaani China kwa kuwa chanzo kikuu cha dawa ya Fentanyl nchini humo. Bw. Liu anasema,

    "Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Marekani, kuanzia Oktoba mwaka jana hadi Machi mwaka huu, nchi hiyo iligundua kesi 229 ya magendo ya dawa ya Fentanyl, na kukamata kilo 536.8 za dawa hiyo, ambapo kati yao, kesi 17 na kilo 5.87 za dawa zinatoka China. Hivyo lawama ya Marekani hailingani na ukweli wa mambo."

    Vyombo vya habari vya Marekani vimesema, sababu kuu ya taabu ya Fentanyl nchini humo ni desturi ya watu wa nchi hiyo. Bw. Liu anasema,

    "Watu wa Marekani wanapenda kutumia dawa ya afyuni, ambapo Wamarekani wanaochukua asilimia 5 ya watu duniani wametumia asilimia 80 ya dawa hiyo duniani."

    Bw. Liu amesema, China siku zote inatetea kupiga marufuku dawa za kulevya, na kupenda kushirikiana zaidi na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, ili kujenga ushirikiano wenye usawa, uaminifu na mafanikio ya pamoja, na kutatua suala sugu la dawa za kulevya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako