Takwimu kutoka kwa kampuni hiyo zinaonyesha kuwa wateja 93,580 wameunganishwa kwenye gridi ya taifa ikilinganishwa na 82,373 iliyounganishwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Inasema ripoti hiyo kwamba viunganisho kwa jumla vilikua kwa asilimia 7.2 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita na kuongeza wigo wa wateja hadi 1.4.
Hata hivyo idadi ya wateja wapya iko chini kuliko lengo la serikali, ambalo mnamo Novemba mwaka jana ilizindua utekelezaji wa sera ya uunganisho wa umeme bila malipo kwa lengo la kuunganisha wateja 300,000 kila mwaka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |