• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani isitoe tena kauli hasi juu ya kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi cha Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-09-03 19:25:38

    China imesema serikali ya mkoa wa Xinjiang imeanzisha kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi, kwa ajili ya kuwaokoa watu waliobadilishwa kimawazo na magadi na hata kujiunga na kundi la kigaidi na kufanya uhalifu mdogo, ili wasiathiriwe vibaya na itikadi kali.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema hayo alipoulizwa kuhusu kauli hasi iliyotolewa hivi karibuni na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kuhusu kituo hicho cha elimu na mafunzo mkoani Xinjiang, China.

    Bw. Geng amesema hivi sasa hali kwenye jamii ya Xinjiang ni tulivu, uchumi unaendelea vizuri, watu wa makabila mbalimbali tofauti wanaishi kwa masikilizano, na hakuna shambulizi la kigaidi lililotokea katika miaka mitatu iliyopita.

    Bw. Geng ameongeza kuwa China inawataka baadhi ya wanasiasa wa Marekani waache kuingilia kati mambo ya ndani ya China na kufanya kazi zinazohimiza hali ya kuaminiana na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako