• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Korea Kaskazini wajadili ushirikiano na hali ya peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2019-09-03 19:30:51

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho wamekutana na kujadiliana juu ya uhusiano wa pande mbili na hali ya Peninsula ya Korea.

    Bw. Wang ambaye yuko ziarani nchini Korea Kaskazini amesema mwaka huu nchi hizi mbili zinaadhimisha miaka 70 tangu kuanzisha uhusiano wao wa kibalozi, na kwamba ziara ya rais Xi Jiping nchini humo aliyoifanya mwezi Juni, ilipata mafanikio makubwa na ni hatua kubwa, ambayo imehimiza zaidi urafiki wa jadi na kuaminiana kimkakati na kuendeleza mbele ushirikiano kati ya pande hizo mbili pamoja na kuzipeleka nchi hizo katika zama mpya.

    Kwa upande wake Bw. Ri amesema nchi yake inachukua juhudi ya kuendelea kuhimiza urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako