• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tume za uchaguzi za Afrika zatakiwa kuimarisha mchakato wa chaguzi zake

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:25:40

  Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Siasa ya Umoja wa Afrika Khabele Matosha jana alitoa wito wa kuimarisha tume za uchaguzi katika Afrika.

  Akiongea kwenye mkutano wa siku mbili wa wakuu wa tume za uchaguzi za Afrika huko mjini Kigali, Rwanda, amesema kutokuwa na imani kwenye mchakato wa uchaguzi ndio sababu ya idadi ya wapiga kura kuwa ndogo katika chaguzi nyingi za Afrika, kwani wananchi wanaona kura zao hazina umuhimu katika kuamua matokeo ya mwisho. Amebainisha kuwa ikiwa kila mwaka kuna mataifa 15 yanayofanya uchaguzi Afrika, baadhi ya mataifa hayo huishia kwenye vurugu zinazopelekea watu kukimbia makazi yao huku mengine yakiwaacha wananchi kwenye dimbwi la machafuko.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Rwanda Kalisa Mbanda amesisitiza kuwa kuna haja ya kuhakikisha ushiriki wa wananchi kwenye utawala na kujenga uongozi unaoaminika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako